Simulizi mpya :

BIOGRAPHY

 
 
Nilizaliwa tarehe 14 october, 1990's katika hospitali ya Muhimbili, ilala jijini Dar es salaam. Baba yangu ndiye alilipenda jina hili la Stallone. Alipenda sinema za Silveter Stallone Rambo kipindi hicho mama yangu ana ujauzito wangu. Mimi nikiwa tumboni kwa mama yangu.
Baba yangu akajisemea
"Nikipata mtoto wa kiume, nitamuita Stallone"

Jumatatu jioni, nikazaliwa nikiwa mtoto wa pili baada ya dada yangu aliyeitwa Diana.

Nilisoma shule ya msingi Kurasini 1998-2004 ikiwa chini ya mwalimu M.J Manoni.

2004 nikapitia kipindi kigumu sana katika maisha yangu. Miezi michache kabla sijafanya mtihani wa kumaliza darasa la saba, mama yangu alifariki akiwa mgonjwa kitandani. Kifo chake kiliniumiza sana. Yeye alikuwa kila kitu kwangu na ndiye alikuwa mzazi wangu wa pekee niliyemtegemea katika maisha yangu.

Nikachaguliwa katika shule ya sekondari Chang'ombe mara baada ya matokeo kutoka, 2005-2008. Huko nikatamani kuja kuwa Daktari siku moja 2007 ndoto hizo zikafutika na kuutamani uandishi wa habari.

2010-2012 nikajiunga na chuo cha uandishi wa habari TsJ kuchukua masomo ya uandishi wa habari pale ilala bungoni. As Advance Diploma.

Mbali na uandishi wa habari niliospecilies katika kuandika magazetini nikiwa nimeshandikia katika magazeti ya UHURU PUBLICATION LTD mimi ni muandishi wa riwaya za kusisimua, upelelezi, uchawi, maisha na mapenzi.

Vitabu ambavyo nimekwisha viandika na kukamilika ni
1-Kivuli cheusi (upelelezi na kisasi)
2-Niliongea na shetani ili niwe tajiri (uchawi)
3-Roho Iliyorudi kuangamiza(kisasi na Maisha)
4-Nenda na Moyo wangu(Mapenzi, Maisha na upelelezi)
5-Usife kabla yangu (mapenzi)
6-Siondoki Mpaka nife (mapenzi)
7-Nisamehe mwanangu (maisha)
8-Kuna kitu kilitokea katika maisha yangu(Maisha)
9-Changudoa(Maisha)
10-Muuaji anayetafutwa (upelelezi na Maisha)
11-Ujumbe wa kifo (upelelezi na kisasi)
12-Malkia wa machozi(Maisha)
13-Nina kiu ya damu(Uchawi)
14-Kijakazi(Maisha)
15-Roho za wafu (nguvu za giza na maisha)
Na nyingine nyingi zaidi ya 24.

Uandishi wa simulizi hizi nimeanza miaka tisa iliyopita mpaka hapa nilipofika. Namshukuru mungu kwa kujizolea mashabiki wengi kwa vitabu ambavyo nimekwishavitoa www.facebook.com/Simulizi02 na kuwa na zaidi ya mashabiki 10,000

Stallone Joyfully
0654846084/0759846084/0684846084
Sjoyfully@gmail.com
Twitter @cooljet91

Post a Comment

BLOG MEMBERS

FACEBOOK PAGE

How many they are online

WALIOTEMBELEA

 

Copyright © 2011. Fanani mpole - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre
Proudly powered by Blogger